×

LingQをより快適にするためCookieを使用しています。サイトの訪問により同意したと見なされます クッキーポリシー.

image

Habari za UN, UNESCO: Urithi wa Kiafrika bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria | | Habari za UN

UNESCO: Urithi wa Kiafrika bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria | | Habari za UN

Ikiwa leo ni siku ya urithi wa dunia wa Afrika, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linasema urithi huo ambao thamani yake ya kipekee inaadhimisha leo, bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria, wa kibinadamu na wa asili.

Taarifa ya Evarist Mapesa inafafanua zaidi.

Kupitia ujumbe wake wa siku hii mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema baada ya kupitishwa mkataba wa urithi wa dunia miaka 50 iliyopita na kuanza kutekelezwa rasmi mwaka 1978, miongoni mwa maeneo 12 ya kwanza kuingizwa kwenye orodha ya urithi wa duniani matatu yalikuwa barani Afrika - hii ikimaanisha kwamba robo ya maeneo ya awali yaliyochaguliwa yalikuwa barani humo.

Hata hivyo amesema “Leo, hii, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara inachukua takriban moja ya kumi ya maeneo yote yaliyoorodheshwa ingawa thamani ya urithi wake wa kipekee, bado haijatambuliwa. Ili kukabiliana na hali hii, na kuupa heshima ipasavyo kutokana na fikra za binadamu na kazi za asili zinazopatikana barani Afrika, UNESCO imeliweka bara hili kuwa kitovu cha mkakati wake wa urithi wa dunia.”

Mkuu huyo wa UNESCO amesisitiza kuwa kuna haja ya kufikiria upya utekelezaji wa mkataba wa urithi wa dunia ili kukabiliana na changamoto zitakazoukabili miaka mingine 50 ijayo na hatimaye kufanikisha msingi wa mkataba huo wa urithi wa kipekee wa dunia nzima.

Ameongeza kuwa “Ni kwa sababu ya upekee wake wa kina, utofauti wake na utajiri wake ndiyo maana urithi wa Kiafrika ni wa ulimwengu wote na unahitaji tuutilie maanani. Mifano ya urithi huu ni pamoja na misikiti minane ya mtindo wa Wasudan nchini Côte d'Ivoire ambayo iliingizwa kwenye orodha ya urithi wa dunia mwaka jana, mbuga ya taifa ya wanyama ya Ivindo Gabon ambayo inahifadhi wanyama wengi walio hatarini kutoweka ikiwemo tembo.”

Azoulay amehitimisha ujumbe wake kwa ahadi kwamba “Ili kutambua vyema urithi huu wa Kiafrika na kuwezesha mchango wake kwa urithi wetu wa dunia, tutahakikisha kwamba kufikia mwaka wa 2025, mataifa yote ya Afrika yanayotaka kufanya hivyo yatakuwa yamewasilisha angalau ombi moja la kujumuishwa kwenye orodha ya urithi wa dunia kwa msaada wa kisayansi na kiufundi kutoka kwa Shirika la UNESCO.”

Shirika hilo linasema “ingawa Afrika ina uwakilishi mdogo kwenye orodha ya urithi wa dunia, mali za Kiafrika zinachukua takribani asilimia 12 ya maeneo yote yaliyoorodheshwa duniani, na asilimia 39 ya mali hizi ziko kwenye orodha ya urithi wa dunia ulio hatarini.”

Ukikabiliwa na vitisho mbalimbali vya kisiasa, mabadiliko ya tabianchi, maendeleo yasiyodhibitiwa, ujangili, machafuko ya kiraia na ukosefu wa utulivu, maajabu mengi ya urithi wa Afrika yana hatari ya kupoteza thamani yake bora ya ulimwengu.

“Kwa hiyo ni suala la dharura zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwamba urithi huu usiweze kubadilishwa ulindwe na kuhifadhiwa kwa ajili ya kufurahiwa na vizazi vijavyo.”

Siku hii huadhimishwa kila mwaka Mei 5 na UNESCO inasema ni fursa kwa watu wote duniani, na hasa Waafrika, kusherehekea urithi wa kipekee wa kitamaduni na wa asili wa bara hilo.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE

UNESCO: Urithi wa Kiafrika bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria | | Habari za UN |||||noch nicht anerkannt|entsprechend||Bedeutung|||||| UNESCO|Heritage||African heritage|still|has not been recognized|according to||importance|||historical significance||| |تراث||||لم يتم التعرف عليه||||||||| |||afrikansk arv||has not been recognized|enligt||betydelse|||historisk||| UNESCO: Afrikanisches Erbe wird immer noch nicht entsprechend seiner historischen Bedeutung anerkannt | UN-Nachrichten UNESCO: African heritage is still not recognized according to its historical importance | UN news UNESCO: Patrimonio africano aún no es reconocido según su importancia histórica | noticias de la ONU یونسکو: میراث آفریقا با توجه به اهمیت تاریخی آن هنوز به رسمیت شناخته نشده است | اخبار سازمان ملل UNESCO : le patrimoine africain n'est toujours pas reconnu selon son importance historique | Nouvelles de l'ONU ユネスコ:アフリカの遺産はその歴史的重要性に応じてまだ認識されていない|国連ニュース UNESCO: Afrikaans erfgoed wordt nog steeds niet erkend op basis van zijn historisch belang | VN-nieuws UNESCO: Dziedzictwo Afryki w dalszym ciągu nie jest rozpoznawane ze względu na jego znaczenie historyczne | Wiadomości ONZ UNESCO: patrimônio africano ainda não é reconhecido por sua importância histórica | notícias da ONU ЮНЕСКО: африканское наследие до сих пор не признано по своей исторической значимости | Новости ООН 联合国教科文组织:非洲遗产因其历史重要性仍未得到承认|联合国新闻

Ikiwa leo ni siku ya urithi wa dunia wa Afrika, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linasema urithi huo ambao thamani yake ya kipekee inaadhimisha leo, bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria, wa kibinadamu na wa asili. ||||||||||Organisation||Bildung|Wissenschaft||Kultur||||Vereinte Nationen||||||Wert|||einzigartigen|feiert||||||||||||||natürliche إذا||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||| "If"|||||heritage|||||organization||education|science||culture||United Nations Organization||||"it says"|heritage|that heritage|which|value|||unique value|is celebrating|||"not recognized yet"|"in accordance with"||importance|||historical significance||"Human significance"|||natural heritage |||||||||||||||kultur||||||säger||||värde|||unika|firasar||||||||||||||ursprung Wenn heute der Welterbetag Afrikas ist, sagt die Bildungs-, Wissenschafts- und Kulturorganisation der Vereinten Nationen (UNESCO), dass dieses Erbe, dessen einzigartiger Wert heute gefeiert wird, immer noch nicht in Übereinstimmung mit seiner historischen, menschlichen und natürlichen Bedeutung anerkannt wird. If today is Africa's world heritage day, the educational, scientific and cultural organization of the United Nations UNESCO says that the heritage whose unique value is being celebrated today, has not yet been recognized according to its historical, human and natural importance.

Taarifa ya Evarist Mapesa inafafanua zaidi. Bericht||||erläutert| Report||Evarist|"Mapesa"|"explains further"| ||Evarist|Evarist Mapesa|förklarar mer| Eine Erklärung von Evarist Mapesa erläutert dies weiter. Evarist Mapesa's statement explains more.

Kupitia ujumbe wake wa siku hii mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema baada ya kupitishwa mkataba wa urithi wa dunia miaka 50 iliyopita na kuanza kutekelezwa rasmi mwaka 1978, miongoni mwa maeneo 12 ya kwanza kuingizwa kwenye orodha ya urithi wa duniani matatu yalikuwa barani Afrika - hii ikimaanisha kwamba robo ya maeneo ya awali yaliyochaguliwa yalikuwa barani humo. |||||||||||||||اعتماد|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||| Durch|Nachricht|||||Generaldirektor|||||||||verabschiedet|Vertrag||||||vor 50 Jahren||beginnen|umgesetzt|offiziell||unter den||Gebiete|||aufgenommen werden||Liste|||||drei||auf dem Kontinent|||||||||ursprünglich ausgewählt|ausgewählt wurden|||dort drüben |message|||||Director||||Audrey Azoulay|Audrey Azoulay||"after" or "since"||"Adoption" or "passing"|Treaty||World heritage sites||||"years ago"||to begin|implemented|officially||among||areas|||included in||list||heritage|||three|"were"|in Africa||this|meaning that||quarter||sites/areas/locations||"initially selected areas"|"were selected"||in Africa|"there" ||||||direktör||||Audrey|Azoulay||||godkännas|avtal|||||||||började genomföras|officiellt|||||||införlivande|||||||||i Afrika|||it means||en fjärdedel|||||som valts||| In ihrer Botschaft an diesem Tag sagte die Generaldirektorin der UNESCO Audrey Azoulay, dass nach der Verabschiedung des Weltkulturerbe-Vertrags vor 50 Jahren und seiner offiziellen Umsetzung im Jahr 1978 unter den ersten 12 Orten, die in die Liste des Weltkulturerbes aufgenommen wurden, drei in Afrika waren - dies bedeutet, dass ein Viertel der ursprünglich ausgewählten Orte in diesem Kontinent lagen. Through his message of this day, the director general of UNESCO, Audrey Azoulay, has said that after the adoption of the World Heritage Convention 50 years ago and its official implementation in 1978, among the first 12 places included in the World Heritage List, three were in Africa, meaning that a quarter of the original selected areas were on the continent.

Hata hivyo amesema “Leo, hii, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara inachukua takriban moja ya kumi ya maeneo yote yaliyoorodheshwa ingawa thamani ya urithi wake wa kipekee, bado haijatambuliwa. Dennoch|trotzdem|||||||Wüste||||etwa|||||||||Wert||||||| |even so|||this||Southern Africa||desert||Sahara Desert|"takes up"|approximately|||||areas|all the areas|listed areas|"even though"|value||heritage|||unique heritage value||not yet recognized ||||||||öken||Sahara|tararika||||||||som är listade|||||||||har inte erkänts Dennoch sagte er, dass heute Afrika südlich der Sahara etwa ein Zehntel aller aufgeführten Stätten ausmacht, obwohl der einzigartige Wert seines Erbes noch nicht anerkannt ist. However, he has said "Today, sub-Saharan Africa occupies approximately one tenth of all listed areas, although the value of its unique heritage has not yet been recognized. Ili kukabiliana na hali hii, na kuupa heshima ipasavyo kutokana na fikra za binadamu na kazi za asili zinazopatikana barani Afrika, UNESCO imeliweka bara hili kuwa kitovu cha mkakati wake wa urithi wa dunia.” |"to address"|||||"to give"|due respect|"appropriately"|"due to"||ideas of humans||human beings|||||"that are found"|"in Africa"|||"has made"||"this"||center||strategy||||| ||||||att ge|respekt, ära, värde|som det bör|||tankar|||||||som finns||||har placerat|bara|||centrum||strategi||||| Um dieser Situation zu begegnen und ihm angemessene Anerkennung zu geben angesichts der Denkweisen und natürlichen Werke, die auf dem afrikanischen Kontinent zu finden sind, hat die UNESCO diesen Kontinent zum Zentrum ihrer Welterbe-Strategie gemacht. To deal with this situation, and to give due respect to the human genius and natural works found in Africa, UNESCO has placed this continent at the center of its world heritage strategy.”

Mkuu huyo wa UNESCO amesisitiza kuwa kuna haja ya kufikiria upya utekelezaji wa mkataba wa urithi wa dunia ili kukabiliana na changamoto zitakazoukabili miaka mingine 50 ijayo na hatimaye kufanikisha msingi wa mkataba huo wa urithi wa kipekee wa dunia nzima. |that UNESCO chief|||"has emphasized"|||need||rethink|"afresh" or "anew"|implementation||treaty||||||address||challenges|will face||"next"|||"ultimately" or "in the end"|achieve|foundation|||||||unique|||whole world ||||harshly emphasized|||behov||||genomförande|||||||||||utmaningar som kommer||||||åstadkomma||||||||||| Der UNESCO-Direktor betonte, dass es notwendig ist, die Umsetzung des Welterbeabkommens zu überdenken, um den Herausforderungen der nächsten 50 Jahre zu begegnen und letztendlich die Grundlage dieses einzigartigen Erbes des gesamten Globus zu verwirklichen. The head of UNESCO has emphasized that there is a need to rethink the implementation of the world heritage convention in order to face the challenges that will be faced in the next 50 years and finally achieve the foundation of the unique world heritage convention.

Ameongeza kuwa “Ni kwa sababu ya upekee wake wa kina, utofauti wake na utajiri wake ndiyo maana urithi wa Kiafrika ni wa ulimwengu wote na unahitaji tuutilie maanani. "Has added"||||||uniqueness|||depth|diversity|||wealth|||reason why|heritage|||||the world|||"requires"|"we consider"|pay attention to har har lagt till||||||unikhet|||djup|mångfald|||rikedom|||anledning||||||världen|||du behöver|vi ska bevara|beakta He added that "It is because of its deep uniqueness, its diversity and its richness that is why the African heritage is universal and needs to be taken into account. Mifano ya urithi huu ni pamoja na misikiti minane ya mtindo wa Wasudan nchini Côte d'Ivoire ambayo iliingizwa kwenye orodha ya urithi wa dunia mwaka jana, mbuga ya taifa ya wanyama ya Ivindo Gabon ambayo inahifadhi wanyama wengi walio hatarini kutoweka ikiwemo tembo.” Examples||heritage|||||mosques|eight||style||Sudanese style||Ivory Coast|Ivory Coast||"was included"||list||heritage||||last year|national park||national park||||Ivindo National Park|Gabon||"protects"|||"who are"|"At risk"|"to disappear"|including|elephants exempel|||||||moskéer|åtta||||wasudan||Elfenbenskusten|Elfenbenskusten||infördes|||||||||national park||||||Ivindo nationalpark|Gabon||bevar|||||utrotas||elefanter Examples of this heritage include the eight Sudanese-style mosques in Côte d'Ivoire that were added to the world heritage list last year, the Ivindo Gabon national zoo which shelters many endangered animals including elephants.

Azoulay amehitimisha ujumbe wake kwa ahadi kwamba “Ili kutambua vyema urithi huu wa Kiafrika na kuwezesha mchango wake kwa urithi wetu wa dunia, tutahakikisha kwamba kufikia mwaka wa 2025, mataifa yote ya Afrika yanayotaka kufanya hivyo yatakuwa yamewasilisha angalau ombi moja la kujumuishwa kwenye orodha ya urithi wa dunia kwa msaada wa kisayansi na kiufundi kutoka kwa Shirika la UNESCO.” |"has concluded"|message|||promise|||"Recognize" or "acknowledge"|properly||||African heritage||enable|contribution|||||||"we will ensure"||by the year|||||||"That wish"|||"will have"|"have submitted"|at least|request|||included||||||||assistance||scientific assistance||technical assistance||||| |har avslutat||||löfte|||erkänna|||||||möjliggöra|bidrag|||||||säkerställa||nå ut|||||||som vill||||har skickat in||ansökan|||inkludering||||||||||||tekniskt||||| Azoulay concluded his message with a promise that "In order to better recognize this African heritage and facilitate its contribution to our world heritage, we will ensure that by the year 2025, all African nations that wish to do so will have submitted at least one request to be included in the heritage list of the world with scientific and technical support from UNESCO."

Shirika hilo linasema “ingawa Afrika ina uwakilishi mdogo kwenye orodha ya urithi wa dunia, mali za Kiafrika zinachukua takribani asilimia 12 ya maeneo yote yaliyoorodheshwa duniani, na asilimia 39 ya mali hizi ziko kwenye orodha ya urithi wa dunia ulio hatarini.” ||||||representation|small representation||||heritage|||heritage sites|||"account for"||percent||||||||||these properties|are listed|||||||"in danger"| ||||||representativ||||||||tillgångar|||utgör|ungefärligt||||||||||||är|||||||| The organization says "although Africa is underrepresented on the world heritage list, African properties account for approximately 12 percent of all listed sites in the world, and 39 percent of these properties are on the list of world heritage in danger."

Ukikabiliwa na vitisho mbalimbali vya kisiasa, mabadiliko ya tabianchi, maendeleo yasiyodhibitiwa, ujangili, machafuko ya kiraia na ukosefu wa utulivu, maajabu mengi ya urithi wa Afrika yana hatari ya kupoteza thamani yake bora ya ulimwengu. Faced with||threats|||political|||climate change|uncontrolled development|uncontrolled development|poaching|civil unrest||civil unrest||lack of||stability|wonders||||||are at risk|risk of losing||lose|value|||| If faced||hotande|||politiskt|förändringar||klimatförändringar|utveckling|okontrollerad utveckling|tjuvjakt|||civila||||stabilitet|underverk|||||||||förlora||||| Faced with various political threats, climate change, uncontrolled development, poaching, civil unrest and instability, many of the wonders of Africa's heritage are at risk of losing their outstanding global value.

“Kwa hiyo ni suala la dharura zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwamba urithi huu usiweze kubadilishwa ulindwe na kuhifadhiwa kwa ajili ya kufurahiwa na vizazi vijavyo.” |||issue||emergency||"than"||"any other time"|"any other time"||||"cannot be"|be altered|"be protected"||"be preserved"||||enjoyment||generations to come|future generations |||fråga|||||||||||må inte|ändras|skyddas||be preserved||||för att njuta||generation|framtida generationer "Therefore, it is more urgent than ever that this heritage cannot be changed, protected and preserved for the enjoyment of future generations."

Siku hii huadhimishwa kila mwaka Mei 5 na UNESCO inasema ni fursa kwa watu wote duniani, na hasa Waafrika, kusherehekea urithi wa kipekee wa kitamaduni na wa asili wa bara hilo. ||is celebrated||||||||||||||especially|Africans|celebrate|||||cultural heritage|||||| ||firande|||maj 5|||||||||||och särskilt|Afrikaner|fira festligt||||||||||| This day is celebrated every year on May 5 and UNESCO says it is an opportunity for all people in the world, and especially Africans, to celebrate the unique cultural and natural heritage of the continent.