×

We gebruiken cookies om LingQ beter te maken. Als u de website bezoekt, gaat u akkoord met onze cookiebeleid.

image

Habari za UN, COVID-19 ilidhihirisha kila mkazi wa dunia ana thamani yake - Susan Mang'eni | | Habari za UN

COVID-19 ilidhihirisha kila mkazi wa dunia ana thamani yake - Susan Mang'eni | | Habari za UN

Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa ajili ya maendeleo 2023 FfD linaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fedha wa kimataifa na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 katika mstari unaotakiwa ikiwa imesalia chini ya miaka saba kufikia ukomo.

Nchi, hususan zinazoendelea zinahaha kuhakikisha zinatimiza malengo yake kwa kila hali na miongoni mwao ni Kenya ambapo Susan Auma Mang'eni Katibu Mkuu wa Idara ya Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo iliyo ndani ya Wizara Mpya ya Ushirika na Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo au Ujasiriamali nchini humo anahudhuria kongamano hilo na amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amekuja na ujumbe maalum kutoka Kenya.

“Kwanza nimekuja hapa ili kuwasilisha ujumbe wetu wa Kenya hasa tunavyoona ufadhili wa maendeleo, kwa sababu lile janga la COVID-19 limedhihirisha bayana kwamba hakuna sehemu yoyote hapa duniani ambayo haina faida ya mambo ya uchumi, hakuna binadamu yeyote ambaye hana uzuri wake, hana thamani ya kiuchumi. Na limeonyesha ya kwamba wakati ule ambao tulikuwa katika zile hekaheka tukijaribu kujiuliza ni jinsi gani tutakabvyoliangamiza hili janga la COVID tulijiuliza maswali lakini hatukuwa na majibu , sasa ilibidi ya kwamba kila sehemu duniani kila nchi ianze kujifikiria kuona ya kwamba ni lipi sisi tunaweza fanya kuangamiza COVID-19. Na tunaona ya kwamba kuna nchi nyingi sana katikia hii dunia ambazo ziliweza kushinda haya madhara ya COVID -19 na sasa hivi imeonesha ya kwamba kama dunia sasa lazima tuanze kujiuliza ni jinsi gani sasa tutakavyoweza kukuza uchumi wetu, ili tuweze kuboresha Maisha ya wananchi wetu ili hapo baadaye litakapotokea tena janga kama hili tusife sana kama jinsi tulivyopoteza wananchi wetu.”

Akaenda mbali zaidi na kusema rasilimali watu ipo wanachohitaji sasa na wanachokiomba kwenye mkutano huu ni ufadhili ili kufikia malengo ya maendeleo na ukuzaji uchumi wao.

“Tunaweza kusema kwamba majibu mengi yako katika urithi wetu kama nchi na hasa sisi hapo Kenya tunatambua ya kwamba urithi wetu uko katika wananchi wetu, kwa watu wetu ambao wana bidii, wana ndoto nzuri na wameonesha kwamba wao wanaweza kufanya lolote ili kuendelea kimaisha. Na tumeona kwamba ukienda popote pale utaona rasilimali ipo, na hii rasilimali utaitambua kupitia utamaduni wetu, jinsi ambayo tunaishi na jinsi ambavyo tunashirikiana na wengine kwa vyakula vyetu, kwa kilimo chetu , kwa bidii yetu, ndio inaonesha kuwa hiyi ndio rasilimali yetu.”

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE

COVID-19 ilidhihirisha kila mkazi wa dunia ana thamani yake - Susan Mang'eni | | Habari za UN COVID|it showed||inhabitant||||||Susan|Mang'eni||| COVID-19 hat gezeigt, dass jeder Bewohner der Welt einen Wert hat – Susan Mang'eni | | UN-Nachrichten COVID-19 showed that every inhabitant of the world has value - Susan Mang'eni | | UN news COVID-19 demostró que cada habitante del mundo tiene valor - Susan Mang'eni | | noticias de la ONU کووید-19 نشان داد که هر ساکن جهان دارای ارزش است - سوزان منگنی | | اخبار سازمان ملل Le COVID-19 a montré que chaque habitant du monde a de la valeur - Susan Mang'eni | | Actualités de l'ONU 新型コロナウイルス感染症は、世界のすべての住民に価値があることを示しました - スーザン・マンゲニ | |国連ニュース 코로나19는 세계의 모든 주민이 가치를 갖고 있음을 보여주었습니다. - Susan Mang'eni | | 유엔 뉴스 COVID-19 pokazał, że każdy mieszkaniec świata ma wartość – Susan Mang'eni | | Wiadomości ONZ A COVID-19 mostrou que cada habitante do mundo tem valor - Susan Mang'eni | | notícias da ONU COVID-19 visade att varje invånare i världen har värde - Susan Mang'eni | | FN-nyheter COVID-19 表明世界上每个居民都有价值 - Susan Mang'eni | |联合国新闻 COVID-19 表明世界上的每个居民都有价值 - Susan Mang'eni | |联合国新闻

Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa ajili ya maendeleo 2023 FfD linaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fedha wa kimataifa na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 katika mstari unaotakiwa ikiwa imesalia chini ya miaka saba kufikia ukomo. Platform||Unity||United Nations||funding||||development|FfD|is ongoing||headquarters|||||||attempt|||system||||international||restoring|agenda|||sustainable|||line|that is required||it remains|||||reaching|limits The United Nations Financing for Development 2023 FfD is underway at the United Nations headquarters in an attempt to transform the global financial system and bring the 2030 sustainable development agenda back on track with less than seven years left to run. Le FfD de financement des Nations Unies pour le développement 2023 est en cours au siège des Nations Unies dans le but de transformer le système financier mondial et de remettre sur les rails le programme de développement durable à l'horizon 2030, alors qu'il reste moins de sept ans.

Nchi, hususan zinazoendelea zinahaha kuhakikisha zinatimiza malengo yake kwa kila hali na miongoni mwao ni Kenya ambapo Susan Auma Mang'eni Katibu Mkuu wa Idara ya Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo iliyo ndani ya Wizara Mpya ya Ushirika na Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo au Ujasiriamali nchini humo anahudhuria kongamano hilo na amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amekuja na ujumbe maalum kutoka Kenya. |especially|developing|are striving||they fulfill|goals||||||||||||Auma||Secretary|Secretary General||||Development|||Small||||Ministry|||cooperative||development|||||Entrepreneurship|||attends|conference|||has informed her|Flora|Nducha||the Department||||she has come||||| Countries, especially developing ones, are trying to ensure that they fulfill their goals in every situation and among them is Kenya where Susan Auma Mang'eni, Secretary General of the Department of Small Business Development within the New Ministry of Cooperatives and Small Business Development or Entrepreneurship in the country is attending a conference that and he has told Flora Nducha of this Kiswahili channel that he has come with a special message from Kenya.

“Kwanza nimekuja hapa ili kuwasilisha ujumbe wetu wa Kenya hasa tunavyoona ufadhili wa maendeleo, kwa sababu lile janga la COVID-19 limedhihirisha bayana kwamba hakuna sehemu yoyote hapa duniani ambayo haina faida ya mambo ya uchumi, hakuna binadamu yeyote ambaye hana uzuri wake, hana thamani ya kiuchumi. |I have come|||to deliver||||||as we see|||||||disaster|||has demonstrated|clearly||||||in the world|||benefit||||economy||||||economic value|||||economic "First of all, I have come here to present our Kenyan message, especially as we see the financing of development, because the COVID-19 epidemic has clearly shown that there is no part of the world that does not benefit from economic matters, there is no human being that does not have its beauty, it has no value economic. Na limeonyesha ya kwamba wakati ule ambao tulikuwa katika zile hekaheka tukijaribu kujiuliza ni jinsi gani tutakabvyoliangamiza hili janga la COVID tulijiuliza maswali lakini hatukuwa na majibu , sasa ilibidi ya kwamba kila sehemu duniani kila nchi ianze kujifikiria kuona ya kwamba ni lipi sisi tunaweza fanya kuangamiza COVID-19. |it has shown|||||||||hustle and bustle|trying|||||we will|||||we asked ourselves|||we were not||answers||||||||||begin|to think about oneself|||||||||destroy| And it has shown that when we were in the upheavals trying to ask ourselves how we are going to destroy this epidemic of COVID, we asked ourselves questions but we had no answers, now it was necessary that every part of the world, every country should start thinking about what we can do to destroy COVID- 19. Na tunaona ya kwamba kuna nchi nyingi sana katikia hii dunia ambazo ziliweza kushinda haya madhara ya COVID -19 na sasa hivi imeonesha ya kwamba kama dunia sasa lazima tuanze kujiuliza ni jinsi gani sasa tutakavyoweza kukuza uchumi wetu, ili tuweze kuboresha Maisha ya wananchi wetu ili hapo baadaye litakapotokea tena janga kama hili tusife sana kama jinsi tulivyopoteza wananchi wetu.” |we see|||||||in this||||were able|overcome||effects||||||has shown|||||||we should||||||we will be able|overcoming||||||||citizens|||||will happen|||||let's not die||||we lost|| And we see that there are many countries in this part of the world that were able to overcome the effects of COVID-19 and now it has shown that as a world now we must start asking ourselves how we will now be able to grow our economy, so that we can improve the lives of our citizens so that Later, when a disaster like this happens again, let's not die as much as we lost our citizens."

Akaenda mbali zaidi na kusema rasilimali watu ipo wanachohitaji sasa na wanachokiomba kwenye mkutano huu ni ufadhili ili kufikia malengo ya maendeleo na ukuzaji uchumi wao. |||||resources|||what they need|||they ask|||||||||||||| He went further and said that human resources are what they need now and what they are asking for at this meeting is funding to achieve the goals of development and development of their economy.

“Tunaweza kusema kwamba majibu mengi yako katika urithi wetu kama nchi na hasa sisi hapo Kenya tunatambua ya kwamba urithi wetu uko katika wananchi wetu, kwa watu wetu ambao wana bidii, wana ndoto nzuri na wameonesha kwamba wao wanaweza kufanya lolote ili kuendelea kimaisha. |||||||heritage|||||||||we recognize||||||||||||||||dream|||have shown||||||||in terms of livelihood "We can say that many answers are in our heritage as a country and especially we in Kenya realize that our heritage is in our citizens, in our people who are hardworking, have good dreams and have shown that they can do anything to continue in life. Na tumeona kwamba ukienda popote pale utaona rasilimali ipo, na hii rasilimali utaitambua kupitia utamaduni wetu, jinsi ambayo tunaishi na jinsi ambavyo tunashirikiana na wengine kwa vyakula vyetu, kwa kilimo chetu , kwa bidii yetu, ndio inaonesha kuwa hiyi ndio rasilimali yetu.” |we have seen|||anywhere||||||||recognize it||culture||||we live||||we collaborate|||||our food||agriculture|our resource|||||it shows||this||| And we have seen that if you go anywhere you will see resources, and you will recognize this resource through our culture, the way we live and the way we cooperate with others with our food, with our agriculture, with our hard work, that shows that this is our resource."