×

Używamy ciasteczek, aby ulepszyć LingQ. Odwiedzając stronę wyrażasz zgodę na nasze polityka Cookie.

image

Habari za UN, UNFPA inasaidia kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake na wasichana wanaokimbia ghasia Khartoum | | Habari za U...

UNFPA inasaidia kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake na wasichana wanaokimbia ghasia Khartoum | | Habari za U...

Wanawake na wasichana wanaokimbia machafuko yanayoendelea mjini Kharthoum nchini Sudan wanakabiliwa na changamoto lukuki hususan kwa wajawazito wanaohitaji msaada wa kujifungua, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambalo sasa limechukua jukumu la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake hao.

Miongoni mwa wanawake hao ni Omnia hili si jina lake halisi amepewa ili kulinda usalama wake, akiwa na ujauzito wa miezi tisa, alilazimika kuacha nyumba yake na kila kitu alichojua ili kuepuka vita kali iliyoukumba mji mkuu wa Sudan, Khartoum kuokoa maisha yake.

Kwa uchumngu mkubwa anasema "Nimepoteza kila kitu katika vita hii. Lakini sikutaka kumpoteza mtoto wangu ambaye bado hajazaliwa.”

Ingawa kusafiri katika hali yake ilikuwa hatari, alihisi hakuwa na chaguo, ukosefu wa usalama, risasi zinazorindima, uporaji na uharibifu wa vituo vya afya ulimaanisha kuwa hakuweza kumuona daktari kwa wiki kadhaa, ilikuwa safari ngumu ya siku tano, hatimaye mapema Juni alifanikiwa kufika Port Sudan, kwenye ufuo wa jimbo la bahari ya Sham.

Omnia alikuwa akilia njia nzima kutoka Khartoum na aliogopa kwamba angepata uchungu na kujifungulia njiani kuelekea Port Sudan.

Kwa mujibu wa UNFPA Omnia ni kisa kimoja tu lakini maelfu ya wanawake na wasichana wanapitia changamoto hiyo hivi sasa Sudan.

Alikuwa na bahati kwani aliwasili katika hospitali ya mafunzo ya Port Sudan ambako alianza kuumwa uchungu na kusaidiwa kujifungua salama mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji.

Hata hivyo UNFPA inasema “hiyo ni hospital pekee ya serikali inayotoa huduma za uzazi kwa watu milioni 1.6 na sasa shirika hilo la idadi ya watu na wadau wa bahari ya Sham wanaisaidia hospitali hio kwa vifaa, dawa na mafunzo kwa wahudumu ili kuhakikisha wakina mama wajawazito kama Omnia waliotawanywa na vita na kuwasili Port Sudan kutoka nchi nzima wanajifungua salama.”

Mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo Dkt. Randa Osman anasema “Timu yetu imejitolea kikamilifu kusaidia wanawake na wasichana wanaowasili kutoka Khartoum, lakini tunahitaji vifaa zaidi vya dharura, ikiwa ni pamoja na mafuta na vifaa vya kuokoa maisha na dawa.

Kwa mujibu wa UNFPA takriban vituo 46 vya afya nchini Sudan vimeshambuliwa, na karibu theluthi mbili havifanyi kazi tena.

Mpango wa hivi karibuni wa msaada wa kibinadamu Sudan unalenga kuwasaidia waty milioni 24.7 ambapo milioni 11 kati yao wanahitaji msaada wa dharura wa huduma za afya na wanawake na wasicha milioni 2.6 miongoni mwao wako katika umri wa kuzaa.

UNFPA inasaidia kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake na wasichana wanaokimbia ghasia Khartoum | | Habari za U... UNFPA trägt dazu bei, eine sichere Geburt für Frauen und Mädchen zu gewährleisten, die vor Gewalt in Khartum fliehen | Neuigkeiten von U... UNFPA helps ensure safe childbirth for women and girls fleeing violence in Khartoum | News of U... El UNFPA ayuda a garantizar un parto seguro para mujeres y niñas que huyen de la violencia en Jartum | Noticias de U... L'UNFPA contribue à garantir un accouchement sans danger pour les femmes et les filles fuyant la violence à Khartoum | Des nouvelles de vous... L’UNFPA aiuta a garantire un parto sicuro per le donne e le ragazze in fuga dalla violenza a Khartoum | Notizie di U... UNFPA、ハルツームで暴力から逃れてきた女性と少女の安全な出産を支援|あなたのニュース UNFPA는 하르툼의 폭력을 피해 도망친 여성과 소녀들의 안전한 출산을 보장합니다. | 당신의 소식 UNFPA helpt een veilige bevalling te garanderen voor vrouwen en meisjes die het geweld in Khartoem ontvluchten | Nieuws van U... UNFPA pomaga zapewnić bezpieczny poród kobietom i dziewczętom uciekającym przed przemocą w Chartumie | Wiadomości o U... UNFPA ajuda a garantir parto seguro para mulheres e meninas que fogem da violência em Cartum | Novidades de vc... ЮНФПА помогает обеспечить безопасные роды для женщин и девочек, спасающихся от насилия в Хартуме | Новости У... UNFPA, Hartum'da şiddetten kaçan kadın ve kızların güvenli doğum yapmasına yardımcı oluyor | Sizden Haberler... 人口基金帮助确保逃离喀土穆暴力的妇女和女童安全分娩|美国新闻...

Wanawake na wasichana wanaokimbia machafuko yanayoendelea mjini Kharthoum nchini Sudan wanakabiliwa na changamoto lukuki hususan kwa wajawazito wanaohitaji msaada wa kujifungua, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambalo sasa limechukua jukumu la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake hao. Women and girls fleeing the ongoing unrest in Khartoum in Sudan are facing serious challenges, especially for pregnant women who need help giving birth, according to the United Nations population and reproductive health organization UNFPA, which has now taken on the responsibility of ensuring safe childbirth for these women. .