Ulijuaje ndugu yako anaishi hapa?
How did you know||||
How did you find out that your brother lived here?
Rafiki alisema kwamba aliishi hapa.
A friend said that he lived here.
Rafiki aliniambia mahali anaishi.
|told me|place|
A friend told me where he lived.
Rafiki alinipa anwani yake.
|gave me|address|
A friend gave me his address.
Unaishi wapi?
you live|
Where do you live?
Naishi na wazazi wangu katika mji mwingine.
I live||my parents|||city|another
I live in my parents' house in another town.
Nyumba ninayoishi, ni ya wazazi wangu.
|I live in||||
The house where I live belongs to my parents.
Na lingine, uliegesha gari lako wapi?
|another|park|||
By the way, where did you park your car?
Niliegesha karibu na kona.
I parked|||corner
I parked around the corner.
Hapakuwa na mahali pa kuegesha karibu na hapa.
There was no|||to park|parking|||
There was no place to park nearer here.
Uliegesha katika upande wa kulia, au upande wa kushoto wa barabara?
||side||right side||||left side||road
Did you park on the right side of the street or on the left side of the street?
Niliegesha upande wa kushoto wa barabara, mbele tu ya shule.
||||||in front|||
I parked on the left side of the street just in front of the school.
Umeegesha kando ya lori kubwa?
parked|side||truck|big
Did you park beside the large truck?
Ndiyo, kwa nini?
Yes I did, why?
Huruhusiwi kuegesha hapo.
not allowed||
You are not allowed to park there.
Mji unakarabati barabara hapo.
|is repairing||
The city is fixing the road there.
Nitaenda na kuhamisha gari langu.
I will go||to move||
I will go and move my car.
Tafadhali nisubiri.
|please wait for me
Please wait for me.
Nina maswali zaidi.
I have some more questions.