×

LingQ'yu daha iyi hale getirmek için çerezleri kullanıyoruz. Siteyi ziyaret ederek, bunu kabul edersiniz: çerez politikası.

image

Habari za UN, Fulgence Kayishema, Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari huenda atahukumiwa nchini Rwanda - Serge Brammertz | | Haba...

Fulgence Kayishema, Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari huenda atahukumiwa nchini Rwanda - Serge Brammertz | | Haba...

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT iliyoko Arusha Tanzania, Serge Brammertz ameeleza kuwa Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, aliyekamatwa juzi Mei ishirini na nne (24) huko Paarl nchini Afrika Kusini huenda akapelekwa nchini Rwanda kukabiliana na mkono wa sheria kutokana na tuhuma za kushiriki kuwaua watu zaidi ya elfu mbili (2000) wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka elfu moja mia tisa tisini na nne (1994). Anold Kayanda amezungumza na Mwendesha Mashitaka huyo na kutuandalia makala ifuatayo.

Ni Mwendesha Mashitaka Mkuu huyo, ofisi ya Mwendesha mashitaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda na Yugoslavia (IRMCT) iliyoko chini ya umoja wa taifa. Anasema kwamba, ndani ya Afrika Kusini pekee, imezichukua takribani mwaka mmoja, mamlaka na kikosi maalum cha umoja wa mataifa kufuatilia mienendo ya Fulgence Kayishema ambapo walitumia takribani miezi kumi kukusanya taarifa kutoka kwa watu ambao walikuwa wanaangaliwa kwamba wanamsaidia mtuhumiwa kujificha na kutoroka mkono wa sheria. Aidha walitumia utaalam wa kisasa wa upelelezi ikiwemo uchambuzi wa mawasiliano ya simu, uchunguzi wa miamala ya kifedha na mbinu nyingine.

Nilipomuuliza kuhusu ni kwa nini imechukua muda mrefu wa zaidi ya miaka ishirini hadi kufikia kumtia mbaroni Fulgence Kayishema, bwana Serge Brammertz anafafanua akisema, "Mojayapo ya shida ni dhahiri kwa watuhumiwa wengi, waliojificha katika nchi za kiAfrika, ni kwamba walitumia vibaya utambulisho bandia na kujificha na hata mara nyingi zaidi kati jamii ya wakimbizi.

Tukimtazama Kayishema kama unavyojua, alihusika kwa kiasi kikubwa katika kufanya mauaji ya kimbari. Kisha akakimbilia DRC. Kutoka hapo akaenda Tanzania, alienda kwenye kambi za wakimbizi huko. Alihamia Msumbiji kwenye kambi nyingine ya wakimbizi. Kisha alikaa muda huko Eswatini kabla mwishoni wa miaka ya tisini kuhamia Afrika Kusini. Wakati huo huo alikua ametumia hati nne tofauti za kusafiria, vitambulisho tofauti, alikuwa hata anapata hati ya ukimbizi wakati huo katika nchi tofauti. Kwa hivyo, hoja ninayotaka kusema ni rahisi sana kupata hati bandia. Ni vigumu sana kwa mamlaka ya kufanya uthibiti wa namna hii. Hasa ikiwa una idadi muhimu ya watuhumiwa walio mafichoni. Na hivyo ndivyo alivyoweza kujificha kwa miaka mingi katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini."

Na kuhusu atakakopelekwa mtuhumiwa huyu wa mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda, Mwendesha Mashitaka Serge Brammertz ananiambia kwamba Afrika Kusini wameanza mchakato wa kisheria. Kisha ombi lililopo ni mtuhumiwa kupelekwa Arusha, Tanzania,

lakini wezekano mkubwa ni kwamba mashitaka na usikilizaji wa kesi itafanyika nchini Rwanda. "Kama unavyojua, tuko katika awamu hii ya mwisho ya ofisi ya Mwendesha Mashitaka ya Mfumo wa Kimataifa wa kushugulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari. Pia, Baraza la Usalama limetuhimiza kuhakikisha kwamba kesi zote zilizosalia zinasikilizwa na ofisi za mashitaka na yeye anayepaswa kufanyiwa hivyo katika taasisi za Rwanda."

Mnamo mwaka wa elfu mbili na moja (2001) Fulgence Kayishema, alishitakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa nchini Rwanda, ICTR, iliyokuwa Arusha, Tanzania kwa makosa ya mauaji ya kimbari, kufanyikisha mauaji ya kimbari, kuchochea mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu kwa mauaji na makosa mengine yaliyofanyika katika kitongoji cha Kivumu, jimbo la Kibuye. Inadaiwa kuwa tarehe kumi na tano (15) mwezi wa Aprili mwaka elfu moja mia tisa tisini na nne (1994), Kayishema pamoja na watuhumiwa wengine, waliwaua zaidi ya watu elfu mbili kwenye kanisa huko Nyange. Na inadaiwa kuwa alishiriki mmoja kwa mmoja katika kupanga na utekelezaji wa mauaji hayo, ikiwa ni kununua na kusambaza petroli na kuchoma moto kanisa ilihali watu wakiwa ndani na hata waliobaki hai bada ya moto walikufa baada ya wauaji hayo kutumia tingatinga kuangusha kanisa lote.

Watuhumiwa wengine watatu bado wanasakwa ili wakutane na mkono wa sheria.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE

Fulgence Kayishema, Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari huenda atahukumiwa nchini Rwanda - Serge Brammertz | | Haba... Fulgence|Kayishema|suspect||genocide||genocide||will be sentenced||||| Fulgence Kayishema, Angeklagter des Völkermords könnte in Ruanda vor Gericht gestellt werden – Serge Brammertz | | Ach nein... Fulgence Kayishema, Accused of genocide may be tried in Rwanda - Serge Brammertz | | Oh no... Fulgence Kayishema, acusado de genocidio puede ser juzgado en Ruanda - Serge Brammertz | | Oh, no... Fulgence Kayishema, accusé de génocide pourrait être jugé au Rwanda - Serge Brammertz | | Oh non... Fulgence Kayishema, acusado de genocídio pode ser julgado em Ruanda - Serge Brammertz | | Oh não...

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT iliyoko Arusha Tanzania, Serge Brammertz ameeleza kuwa Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, aliyekamatwa juzi Mei ishirini na nne (24) huko Paarl nchini Afrika Kusini huenda akapelekwa nchini Rwanda kukabiliana na mkono wa sheria kutokana na tuhuma za kushiriki kuwaua watu zaidi ya elfu mbili (2000) wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka elfu moja mia tisa tisini na nne (1994). Prosecutor|prosecution|Chief Prosecutor||office||Prosecutor General|Prosecutor's Office||system of||international system||dealing with|remains||cases||genocide|of|genocide||located in|Arusha Tanzania||Brammertz|Serge Brammertz|has stated||Fulgence Kayishema|Fulgence Kayishema|||suspects|top suspects|who were|most wanted|||involvement||murders||genocide|||arrested|the day before|May|twenty-four||twenty-four|in|Paarl South Africa|||South Africa|may|may be sent|||face||arm of the law||law|due to||allegations||participating in|||||||||genocide||genocide|||||||||| The Chief Prosecutor of the prosecutor's office of the International Residual Mechanism for Criminal Tribunals, IRMCT located in Arusha Tanzania, Serge Brammertz has explained that Fulgence Kayishema, one of the leading suspects who was most wanted for involvement in the genocide in Rwanda, who was arrested the other day on May twenty-four (24) in Paarl in South Africa may be sent to Rwanda to face the hand of the law due to suspicions of participating in killing more than two thousand (2000) people during the genocide in Rwanda in the year one thousand nine hundred and ninety and four (1994). Anold Kayanda amezungumza na Mwendesha Mashitaka huyo na kutuandalia makala ifuatayo. Anold Kayanda|Anold Kayanda|has spoken||||||prepare us|article|following article Anold Kayanda has spoken to the Prosecutor and prepared the following article for us.

Ni Mwendesha Mashitaka Mkuu huyo, ofisi ya Mwendesha mashitaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda na Yugoslavia (IRMCT) iliyoko chini ya umoja wa taifa. ||||that||||Prosecutor's Office||international tribunal||international system||addressing|remains of||case||of genocide||genocide||||Yugoslavia tribunal||located|||United Nations||United Nations It is the Chief Prosecutor, the Prosecutor's office of the international system for dealing with the remnants of the genocide cases of Rwanda and Yugoslavia (IRMCT) located under the unity of the nation. Anasema kwamba, ndani ya Afrika Kusini pekee, imezichukua takribani mwaka mmoja, mamlaka na kikosi maalum cha umoja wa mataifa kufuatilia mienendo ya Fulgence Kayishema ambapo walitumia takribani miezi kumi kukusanya taarifa kutoka kwa watu ambao walikuwa wanaangaliwa kwamba wanamsaidia mtuhumiwa kujificha na kutoroka mkono wa sheria. |||||South Africa|only|has taken|approximately|year||authorities||task force|special unit|||||monitoring|trends||Fulgence Kayishema|Fulgence Kayishema|where|used||months||gathering|information||||who||are being watched||they are helping|the suspect|hiding||escape|||law He says that, within South Africa alone, it has taken the authorities and the United Nations special force about a year to track the movements of Fulgence Kayishema where they spent about ten months gathering information from people who were being watched that they were helping the suspect to hide and escape the law. Aidha walitumia utaalam wa kisasa wa upelelezi ikiwemo uchambuzi wa mawasiliano ya simu, uchunguzi wa miamala ya kifedha na mbinu nyingine. Additionally|they used|expertise||||investigation|including|analysis||communication analysis|of mobile|phone communications|investigation||financial transactions||financial transactions||methods| In addition, they used modern intelligence expertise, including the analysis of mobile communications, the investigation of financial transactions and other methods.

Nilipomuuliza kuhusu ni kwa nini imechukua muda mrefu wa zaidi ya miaka ishirini hadi kufikia kumtia mbaroni Fulgence Kayishema, bwana Serge Brammertz anafafanua akisema, "Mojayapo ya shida ni dhahiri kwa watuhumiwa wengi, waliojificha katika nchi za kiAfrika, ni kwamba walitumia vibaya utambulisho bandia na kujificha na hata mara nyingi zaidi kati jamii ya wakimbizi. When I asked|||||it has taken||||||||until|reaching|put him|in prison|||Mr|||explains|he says|One of the||problem||||the suspects|many suspects|those in hiding|||||||||identification|fake identity||hiding||||||among|community of refugees||refugee community When I asked him about why it took more than twenty years to arrest Fulgence Kayishema, Mr. Serge Brammertz explains saying, "One of the problems is obvious for many suspects, who are hiding in African countries, is that they misused fake identities and hide and even more often among the refugee community.

Tukimtazama Kayishema kama unavyojua, alihusika kwa kiasi kikubwa katika kufanya mauaji ya kimbari. When we look|||you know|||a large extent|large extent||||| If we look at Kayishema as you know, he was largely involved in committing genocide. Kisha akakimbilia DRC. |he ran to| Then he fled to DRC. Kutoka hapo akaenda Tanzania, alienda kwenye kambi za wakimbizi huko. |from there|he went||||camp||refugee camps| From there he went to Tanzania, he went to the refugee camps there. Alihamia Msumbiji kwenye kambi nyingine ya wakimbizi. He moved|||camp|another||refugees He moved to another refugee camp in Mozambique. Kisha alikaa muda huko Eswatini kabla mwishoni wa miaka ya tisini kuhamia Afrika Kusini. |stayed|||Eswatini|before|at the end||||the nineties|moving to||South He then spent some time in Eswatini before moving to South Africa in the late nineties. Wakati huo huo alikua ametumia hati nne tofauti za kusafiria, vitambulisho tofauti, alikuwa hata anapata hati ya ukimbizi wakati huo katika nchi tofauti. |||he had|has used|documents||||traveling documents|identification documents||||he was obtaining|document||refugee document||at that time||| At the same time, he used four different passports, different identifications, he was even getting an asylum document at that time in different countries. Kwa hivyo, hoja ninayotaka kusema ni rahisi sana kupata hati bandia. ||point|that I want|||easy|||document|fake So, the point I want to make is that it is very easy to find fake documents. Ni vigumu sana kwa mamlaka ya kufanya uthibiti wa namna hii. |difficult|||authorities|||regulation||this type| Hasa ikiwa una idadi muhimu ya watuhumiwa walio mafichoni. especially if|||number|important number||suspects|who are|in hiding Especially if you have a significant number of suspects in hiding. Na hivyo ndivyo alivyoweza kujificha kwa miaka mingi katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini." ||that|he was able|hide himself||years||||||East Africa||Southern And that's how he was able to hide for many years in East and South African countries."

Na kuhusu atakakopelekwa mtuhumiwa huyu wa mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda, Mwendesha Mashitaka Serge Brammertz ananiambia kwamba Afrika Kusini wameanza mchakato wa kisheria. |about|where he will be taken|the suspect|this||of genocide||genocide||||Prosecutor|Prosecutor|||tells me|||South Africa|they have begun|process||legal process And about where this Rwandan genocide suspect will be taken, Prosecutor Serge Brammertz tells me that South Africa has started the legal process. Kisha ombi lililopo ni mtuhumiwa kupelekwa Arusha, Tanzania, Then|request|||the suspect|to be taken|Arusha (1)| Then the current request is for the suspect to be sent to Arusha, Tanzania,

lakini wezekano mkubwa ni kwamba mashitaka na usikilizaji wa kesi itafanyika nchini Rwanda. ||high|||charges||hearing|||will take place|| but the greatest possibility is that the prosecution and hearing of the case will take place in Rwanda. "Kama unavyojua, tuko katika awamu hii ya mwisho ya ofisi ya Mwendesha Mashitaka ya Mfumo wa Kimataifa wa kushugulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari. |as you know|we are||phase 1|||final||||Prosecutor|Prosecutor's Office||System 1||International System||handle|remains of||||genocide cases||genocide "As you know, we are in this final phase of the Office of the Prosecutor of the International System of dealing with the remains of genocide cases. Pia, Baraza la Usalama limetuhimiza kuhakikisha kwamba kesi zote zilizosalia zinasikilizwa na ofisi za mashitaka na yeye anayepaswa kufanyiwa hivyo katika taasisi za Rwanda." |Council|||has urged us|ensure that||||remaining cases|||||prosecution office||he|who should||||institutions|| Also, the Security Council has encouraged us to ensure that all the remaining cases are heard by the prosecution offices and those who should do so in Rwandan institutions."

Mnamo mwaka wa elfu mbili na moja (2001) Fulgence Kayishema, alishitakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa nchini Rwanda, ICTR, iliyokuwa Arusha, Tanzania kwa makosa ya mauaji ya kimbari, kufanyikisha mauaji ya kimbari, kuchochea mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu kwa mauaji na makosa mengine yaliyofanyika katika kitongoji cha Kivumu, jimbo la Kibuye. In the year|year||||||||||||international court||crime||||International Criminal Tribunal|that was||||charges||||genocide|facilitating genocide|committing genocide|||inciting|||genocide||against humanity|against||humanity||and other crimes||charges||||neighborhood||Kivumu (1)|district||Kibuye District In the year two thousand and one (2001), Fulgence Kayishema, was accused by the International Criminal Tribunal for Rwanda, ICTR, which was in Arusha, Tanzania for crimes of genocide, committing genocide, inciting genocide and crimes against human for murder and other crimes committed in Kivumu township, Kibuye province. Inadaiwa kuwa tarehe kumi na tano (15) mwezi wa Aprili mwaka elfu moja mia tisa tisini na nne (1994), Kayishema pamoja na watuhumiwa wengine, waliwaua zaidi ya watu elfu mbili kwenye kanisa huko Nyange. It is alleged||date||||||April||||||||||||suspects|others|they killed||||||||there|Nyange It is alleged that on the fifteenth (15th) of the month of April in the year one thousand nine hundred and ninety four (1994), Kayishema together with other suspects, killed more than two thousand people in a church in Nyange. Na inadaiwa kuwa alishiriki mmoja kwa mmoja katika kupanga na utekelezaji wa mauaji hayo, ikiwa ni kununua na kusambaza petroli na kuchoma moto kanisa ilihali watu wakiwa ndani na hata waliobaki hai bada ya moto walikufa baada ya wauaji hayo kutumia tingatinga kuangusha kanisa lote. |it is alleged|||||||planning||implementation||the murders|those|including||||distributing|petrol||setting fire to||church|while||being||||those who remained|alive|after|||they died|||the murderers|those|using a bulldozer|bulldozer|topple|the church|the whole church And it is alleged that he participated one by one in the planning and execution of the murder, buying and distributing gasoline and burning the church while people were inside and even those who survived the fire died after the killers used bulldozers to demolish the entire church.

Watuhumiwa wengine watatu bado wanasakwa ili wakutane na mkono wa sheria. suspects|others|||are being sought||meet|||| Three other suspects are still wanted to face the law.